• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yafuta amri ya kupiga marufuku vifaa vya kielektroniki kuingia katika ndege zinazotoka Misri

    (GMT+08:00) 2017-07-12 18:44:53

    Shirika la ndege la Misri limethibitisha kuwa Marekani itafuta amri ya kupiga marufuku vifaa vya kielektroniki kuingia katika ndege zinazotoka nchini humo kwenda Marekani.

    Taarifa ya Shirika hilo imesema, uamuzi huo utaanza rasmi leo na muda utatekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja. Waziri wa usafiri wa anga nchini Misri Bw. Sharif Fathi amepongeza uamuzi huo wa Marekani.

    Mwezi wa Machi mwaka huu, Wizara ya ulinzi ya Marekani ilitangaza kuwa kutokana na tishio la kigaidi, Marekani imepiga marufuku vifaa vya kielekotroniki kuingia katika ndege zisizo za mashirika ya ndege ya Marekani kutoka viwanja 10 vya ndege katika nchi 8 za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako