• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasitisha uamuzi wa kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan

    (GMT+08:00) 2017-07-12 18:45:15

    Marekani imeongeza kipindi cha ukaguzi kwa miezi mitano zaidi ili kuamua kama itaondoa kabisa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Sudan.

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema, nchi hiyo imetambua mchakato mzuri uliofanywa na Sudan, lakini bado inahitaji muda zaidi kuthibitisha kuwa nchi hiyo imetatua kihalisi mambo yanayotiliwa mashaka nayo.

    Hatua zenye ushawishi mzuri zinazotarajiwa na Marekani ni pamoja na kumaliza mapigano ya ndani ya kutumia silaha nchini Sudan, kuboresha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na kuhakikisha ushirikiano katika kutatua migogoro ya kikanda na tishio la kigaidi.

    Muda wa mwisho kwa serikali ya Marekani kuamua kama uamuzi wa kuondoa vikwazo uliofikiwa miezi sita iliyopita na serikali ya Obama unamalizika hii leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako