• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya juhudi za kutatua mgogoro wa Bahari ya Kusini kwa njia ya amani

    (GMT+08:00) 2017-07-12 19:00:02

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, China inalinda kithabiti mamlaka ya umiliki wa Bahari ya Kusini na maslahi ya China katika bahari hiyo, na China siku zote inafanya juhudi za kutatua migogoro inayohusika kwa njia ya mazungumzo na nchi zinazohusika.

    Bw. Geng amesema hayo alipozungumzia taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya mambo ya nje ya Philippines kuhusu maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutolewa kwa hukumu kuhusu kesi ya Bahari ya Kusini, ambapo wachambuzi wanaona kuwa taarifa hiyo imeonesha msimamo wa upendeleo.

    Na msemaji huyu alipojibu swali kuhusu jeshi la China kuanzisha kituo cha uhakikisho nchini Djibouti, amesema jambo hili ni uamuzi uliofanywa na serikali za China na Djibouti baada ya majadiliano ya kirafiki. Amesema kuanzishwa kwa kituo hiki kinasaidia China kutekeleza majukumu ya kulinda meli katika ghuba ya Aden na bahari ya Somalia na kufanya uokoaji wa kibinadamu, pia kinasaidia kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na jamii ya Djibouti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako