• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing kuongeza kasi ya kufungua zaidi sekta ya huduma

    (GMT+08:00) 2017-07-12 19:16:31

    Baraza la Serikali la China limeidhinisha mpango wa majaribio wa kufungua zaidi sekta ya huduma kwa mji wa Beijing kwa kuondoa vikwazo zaidi katika sekta hiyo.

    Baraza hilo limesema, mpango huo utakaodumu kwa miaka mitatu, unalenga kuifanya sekta ya huduma katika mji huo mkuu kuwa ya kisasa na ya ngazi ya juu zaidi. Mpango huo unaainisha maeneo muhimu ya kufanyiwa mageuzi, ikiwa ni pamoja na huduma katika sekta ya sayansi na teknolojia, mtandao wa internet na mawasiliano, utamaduni, elimu, pamoja na mambo ya fedha na utalii.

    Mamlaka ya mji wa Beijing itaondoa vikwazo katika uwekezaji, kuruhusu mitaji zaidi ya kigeni, na kurekebisha kanuni na kushawishi uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako