• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Msumbiji atarajia kuimarisha ushirikiano na China

    (GMT+08:00) 2017-07-12 19:17:18

    Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji amesema nchi yake inatarajia kuimarisha ushirikiano na China katika sekta mbalimbali, ikiwemo ulinzi na usalama.

    Rais Nyusi amesema hayo alipokutana na mjumbe wa taifa la China ambaye pia ni waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Chang Wanquan aliyeko ziarani nchini humo. Rais Nyusi pia amesema Msumbiji inathaminisana uhusiano wake na China, na inashikilia kanuni ya uwepo wa China moja, na iko tayari kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na China katika masuala ya kikanda na kimataifa.

    Kwa upande wake, waziri Chang amesema ziara yake inalenga kutimiza makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kuweka msingi wa uhusiano wa pande mbili, na pia kuboresha ushirikiano kati ya nchi hizo. Amesema China inaweka umuhimu mkubwa kwa uhusiano wa nchi hizo mbili na majeshi yao, na iko tayari kujenga jamii yenye hatma ya pamoja na watu wa Msumbiji kwa manufaa ya watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako