• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • East Africa: Kutuma fedha kuenda Tanzania ndiyo ghali sana katika Afrika Mashariki Ripoti inaonyesha

    (GMT+08:00) 2017-07-12 19:54:28

    Kutuma fedha kuenda Tanzania ndiyo ghali sana katika Afrika Mashariki na Kusini, hii ni kulinagna na Ripoti ya kimataifa ya Juni iliyotolewa na Shirika la Ushauri London, na Chama cha Masoko.

    Kulingana na uchambuzi mpya ambao uliwasilishwa katika mkutano wa Mobile 360, ni kwamba gharama ya wastani ya kutuma pauni 120 kutoka Uingereza hadi Tanzania ni asilimia 14, gharama kubwa zaidi katika eneo hilo.

    Zaidi ya pauni milioni 44 hutumwa kila mwaka na Watanzania zaidi ya 38,500 wanaoishi Uingereza lakini gharama ya kutuma fedha ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na kutuma pesa Kenya au Zimbabwe.

    Uchambuzi unaonyesha kwamba gharama ya wastani ya kutuma pesa Afrika ni karibu asilimia 10, ikilinganishwa na wastani wa kimataifa wa zaidi ya asilimia saba.

    Hata hivyo Malengo ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa yanayasema kuwa kufikia mwaka wa 2030 bei ya wastani ya hutumaji fedha haipaswi kuzidi asilimia tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako