• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mapato ya serikali yafikia trilioni 14/-

  (GMT+08:00) 2017-07-12 19:54:44

  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuwa yalikuwa Sh trilioni 14.4.

  Makusanyo hayo yana ongezeko la asilimia 7.67 katika mwaka wa fedha wa 2015/16 ambayo yalikuwa Sh trilioni 13.3.

  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi, Richard Kayombo amesema Juni walikusanya kiasi cha Sh trilioni 1.37.

  Kayombo pia amesema mamlaka imeendelea kukusanya kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo na mwitikio wake umekuwa ni wa kiwango cha kuridhisha.

  TRA pia imetoa wito kwa wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki (EFDs) pindi wanapouza bidhaa .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako