• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Mfumuko wa bei wa Rwanda umeshuka hadi asilimia 4.8 mwezi Juni

    (GMT+08:00) 2017-07-12 19:55:05

    Mfumuko wa bei wa Rwanda umeshuka hadi asilimia 4.8 mwezi Juni ikilinganishwa na asilimia 6.5 iliyoandikwa Mei, Taasisi ya Taifa ya Takwimu ya Rwanda (CPI) inaonyesha.

    Hata hivyo, hii ni ya juu kuliko asilimia 4.1 iliyoandikwa wakati kama huo mwaka jana.

    Kwa mujibu wa ripoti, kushuka kwa mfumuko wa bei kulisababishwa na kupungua kwa bei ya chakula na vinywaji tamu kwa asilimia 9.8 mwezi Juni, chini kutoka asilimia 14.3 iliyandikishwa Mei 2017.

    Vile vile, kodi za makazi, maji, umeme, gesi, usafiri, na mafuta imeongezeka kwa asilimia 1.5 na asilimia 4.6.

    Kiwango cha chini cha mfumuko wa bei, ukiondoa chakula na nishati, ilikuwa imara kila mwezi na iliongezeka kwa asilimia 4.0 ikilinganishwa na mwezi Juni 2016.

    Kiwango cha wastani kati ya Juni 2016 na Juni 2017 kilikuwa asilimia 6.8.

    Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Taifa ya Takwimu ya Rwanda NISR, bei za bidhaa za ndani ziliongezeka kwa asilimia 4.3 kwa mwaka hadi mwaka, lakini ilipungua kwa asilimia 1.1 kila mwezi, wakati bei za "bidhaa za nje" ziliongezeka kwa asilimia 6.4 mwaka hadi mwaka.

    Bei ya "bidhaa za sokoni" iliongezeka kwa asilimia 6.9 kwa mabadiliko ya kila mwaka na ilipungua kwa asilimia 3.8 kila mwezi.

    Benki kuu inakadiria mfumuko wa bei mwaka 2017 utakuwa chini ya asilimia 5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako