• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan asimamisha kamati ya majadiliano na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:07:17

    Rais Omar Al Bashir wa Sudan ametoa amri ya kusimamisha kamati ya majadiliano na Marekani hadi Oktoba 12 mwaka huu, kufuatia uamuzi wa serikali ya Marekani kuahirisha siku ya mwisho ya kufanya uamuzi wa kuiondolea vikwazo Sudan kwa miezi mitatu.

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw Ibrahim Ghandour amesema Sudan imesikitishwa na uamuzi wa Marekani wa kuahirisha kuondoa vikwazo visivyo vya haki, na haijaona sababu ya Marekani kufanya hivyo.

    Mwaka jana Sudan na Marekani zilifikia makubaliano yenye masharti yaliyowekwa na serikali ya Obama. Marekani ilikubali kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan kama nchi hiyo itatimiza masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na kuboresha hali ya haki za binadamu, kusaidia mchakato wa amani Sudan Kusini, na kushirikiana na CIA kupambana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako