• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gor Mahia yawasili Dar es Salam tayari kwa mchuano na Everton

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:20:17
    Mabingwa wa SportPesa Super Cup timu ya Gor Mahia ya Kenya imewasili Dar es Salaam ikitokea Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton ya England ambao wanakuja kwa mara ya kwanza Tanzania.

    Gor Mahia ambao watacheza na kikosi cha kwanza cha Everton hapo kesho uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki, wamewasili wakiwa na mastaa wao wote akiwemo Jean Baptiste Mugiraneza aliyekuwa anaichezea Azam FC.

    Gor Mahia kwa sasa wanafundishwa na kocha wa zamani wa Simba muingereza Dylan Kerr ambaye kwa sasa ndio kocha mkuu na amesema mchezo dhidi ya Everton hautakuwa rahisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako