• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Amavubi anatarajia ushindi dhidi ya Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:20:35
    Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Rwanda Antoine Hey amesema kuwa Amavubi ingependa kusajili matokeo bora dhidi ya Tanzania kwenye mchuano wa kufuzu mashindano ya CHAN mwaka 2018, mkondo wa kwanza, Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

    Mkufunzi huyo kutoka Ujerumani anaamini kuwa kikosi chake sasa kiko katika nafasi nzuri ya kushinda Tanzania kwa sababu wachezaji wanaoibuka wameonyesha shauku ya mafanikio.

    Hey amepewa jukumu la kuhakikisha timu ya Rwanda imefuzu kwa mashindano ya CHAN 2018 na fainali za AFCON 2019 zitakazoandaliwa nchini Kenya na Cameroon kwa mtiririko huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako