• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya Rugby ya Uganda yaonywa dhidi ya utepetevu

  (GMT+08:00) 2017-07-13 09:20:53
  Rugby Cranes ya Uganda wamekuwa na mwanzo bora katika michuano ya African Gold Cup, kwani wameshinda na kutoka sare dhidi ya Senegal na Kenya kwa usanjari huo.

  Lakini timu hiyo imesajili maokeo yasiyo ya kupendeza kwani imeshuka hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi sita, moja nyuma ya Kenya inayoshikilia nafasi ya pili huku Namibia ikijipata kileleni mwa jedwali baada ya kuzamisha senegal 95-0.

  Uganda Jumamosi itacheza na timu ya Tunisia, ambayo hadi sasa haijashinda mchuano wowote katika kundi hilo baada ya kurindimwa na Kenya 110-10.

  Matokeo hayo yanaipa Rugby cranes ya Uganda upato dhidi ya Tunisia lakini kocha wake ameonya wachezaji dhidi ya utepetevu iwapo wanataka kusajili ushindi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako