• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usajili: Hatimaye James Rodriguez akigura Real Madrid

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:21:29
    Mchezaji nyota wa Real Madrid James Rodriguez amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea kwa mkopo mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich ambako ataungana kwa mara nyingine na Meneja Carlo Ancelotti.

    Rodriguez ambaye alitajwa sana kuwindwa na klabu kadhaa za Ulaya ikiwemo Manchester United ya England atafanya vipimo vya afya na miamba ya soka la Ujerumani kabla ya kukamilisha uhamisho kutua Allianz Arena – katika dili abalo linaweza kufikia hadi paundi milioni 40.

    Bayern Munich pia watakuwa na hiyari ya kumnunua moja kwa moja staa huyo wa Kimataifa wa Colombia mwishoni mwa mkataba wake wa mkopo ambapo itakuwa June 30, 2019. Gharama ya mkopo ni paundi milioni 9 wakati kutakuwa na nyongeza ya paundi milioni 31 juu yake kama watamhitaji moja kwa moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako