• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya Marekani vyafuatilia mawasiliano kati ya Trump na Russia wakati wa uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:33:34

    Msemaji wa ikulu ya Russia Bw. Dmitry Peskov amesema, kukutana kwa marais wa Marekani na Russia kumesababisha vyombo vya habari vya Marekani kufuatilia mawasiliano kati ya timu ya kampeni ya rais Trump na Russia wakati wa uchaguzi.

    Amesema baada ya marais hao kukutana tarehe 7 wakati wa mkutano wa kilele wa G20 mjini Hamburg, vyombo vya habari vya Marekani vilianza tena kuripoti mawasiliano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Russia. Amesema ripoti hizo ni mambo ya siasa za ndani za Marekani, na Russia hataki kujihusisha.

    Kuhusu jambo la mtoto wa Bw Trump kukutana na wakili wa Russia Natalia Veselnitskaya, Bw. Peskov amesema, wakili huyo si mwakilishi wa Russia, na kuchunguza suala hilo hakuna msingi wowote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako