• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yawaajiri watumishi wapya wa umma zaidi ya elfu kumi

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:43:51

    Serikali ya Tanzania imetangaza kuwaajiri watumishi wapya wa umma 10,184 ili kuziba pengo lililoachwa na watumishi waliofukuzwa kazi kutokana na vyeti feki mwezi Aprili.

    Waziri wa utumishi wa umma na utawala bora wa Tanzania Bibi Angela Kairuki, amesema serikali ya Tanzania imetoa idhini kwa mabaraza ya wilaya na taasisi nyingine za umma kuwaajiri watumishi wapya, ambao wanatakiwa kuanza kazi tarehe mosi mwezi ujao.

    Mwezi April Rais John Magufuli aliwafuta kazi watumishi wa umma 9,932 waliokutwa na vyeti feki.

    Rais Magufuli ameamuru kwamba watumishi wengine wa umma waliokutwa na vyeti feki wanatakiwa kufikishwa mahakamani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako