• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 5 wafariki katika mashambulizi Mogadishu

    (GMT+08:00) 2017-07-13 09:52:09

    Watu 5 wameuawa na wengine 9 wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili yaliyotokea jana mjini Mogadishu, Somalia.

    Ofisa wa polisi wa Mogadishu Hassan Malim amesema, gari lililokuwa na mabomu lilipuka katika kituo cha ukaguzi kusini mwa mji huo na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 7 kujeruhiwa.

    Siku hiyohiyo, msemaji wa serikali ya Mogadishu, Abdifitah Omar Halane amesema, wapiganaji wanne waliokuwa kwenye gari walikifyatulia risasi kituo cha ukaguzi mashariki mwa mji huo na kusababisha vifo vya watu wawili,, na askari wengine wawili walijeruhiwa.

    Hivi sasa, hakuna kundi lolote linalotaja kuhusika na mashambulizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako