• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawasiliano ya kawaida ya uchumi na biashara kati ya China na Korea Kaskazini hayakiuki uamuzi wa Baraza la Usalama

    (GMT+08:00) 2017-07-13 18:20:55

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, vikwazo vilivyowekewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea ya Kaskazini si vya pande zote, na mawasiliano ya kawaida ya uchumi na biashara kati ya China na Korea Kaskazini hayakiuki uamuzi wa Baraza hilo.

    Takwimu zilizotolewa na Idara kuu ya forodha ya China zimeonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya uuzaji wa bidhaa za China nchini Korea Kaskazini ilikuwa dola za kimarekani bilioni 2.55, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.5. Bw. Geng Shuang amesema, azimio namba 2321 la Baraza la Usalama linasema, chuma na mawe yenye madini ya chuma yanayouzwa nchini Korea Kaskazini yanatumiwa kwa madhumuni ya maisha ya watu, hivyo hazihusiki na vikwazo hivyo. Amesema China inashikilia kithabiti msimamo wa kuhimiza Peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako