• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini kufanya mkutano wa mafuta mwezi Oktoba

    (GMT+08:00) 2017-07-13 18:36:55

    Sudan Kusini kwa kushirikiana na Shirika la Mafuta na Nishati la Afrika AOP itafanya mkutano wa kwanza wa mafuta na nishati mwezi Oktoba, ili kuendeleza sekta ya nishati nchini humo.

    Mkutano huo utakaofanyika mjini Juba utajadili mada mbalimbali ikiwemo usalama, ugavi, teknolojia na uwekezaji. Kwa mujibu wa shirika hilo, mkutano huo pia utachunguza uwezo wa nchi hiyo, kuunga mkono miundombinu ikiwemo barabara, mawasiliano ya simu, faida zinazotokana na gesi, uwekezaji wa nishati pamoja na utandawazi wa kikanda.

    Asilimia 98 ya bajeti ya Sudan Kusini, ambayo ina maliasili nyingi ya mafuta inatengemea faida zinazotokana na mafuta, lakini uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoanza mwezi wa Desemba mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako