• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Rais wa Uganda asema lazima aidhinishe mikopo ya serikali binafsi

    (GMT+08:00) 2017-07-13 18:54:16

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba mikopo yyote ya serikali lazima iidhinishwe naye binafsi kabla hata ya kuwasilisha ombi bungeni.

    Kwenye barua aliomwandikia spika wa bunge Rebecca Kadaga rais Museveni ametaka mikopo 11 ya serikali ikataliwe bungeni akisema kuwa haina manufaa yoyote kwa uchumi wa nchi hiyo.

    Museveni wakati huo huo ameidhinisha kupitishwa kwa mikopo 16 na kusema ni mikopo ya kufadhili miundo mbinu ya elimu na afya inayostahili kufadhiliwa kwa mikopo.

    Baadhi ya mikopo aliofutilia mbali Museveni ni pamoja na ule wa dola milioni 200 wa kujenga barabara ya Kampala-Jinja na nyinbgine ya dola milioni 100 kutoka kwa benbki ya Kiislam ya kupunguza umaskini.

    Taakwimu zilizotolewa na waziri wa fedha Matia Kasaijja zinaonyesha kwamba deni la Uganda la ndani nan je ni zaidi ya dola bilioni 8 kufikia desemba 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako