• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Usajili wa Biashara kufanywa mtandaoni Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-07-13 18:58:21

    Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini Tanzania (Brela) unatarajia kuzindua mfumo wa usajili wa kampuni na biashara kwa njia ya mtandao.

    Baada ya mchakato wa muda mrefu, mfumo huo utazinduliwa mwezi ujao lakini kila Mtanzania anapaswa kuwa na kitambulisho kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) ili kuhudumiwa kwa urahisi.

    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi amesema wageni kutoka nje ya nchi wanatakiwa kutumia namba za pasi zao za kusafiria.

    Awali, huduma ya mtandao ilikuwa ni kwa ajili ya majina ya biashara lakini sasa imepanuliwa na kuruhusu usajili wa majina ya kampuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako