• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka uwajibikaji katika matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria

    (GMT+08:00) 2017-07-13 18:58:17

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka wahusika wa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria wawajibike.

    Bw. Guterres amesema hayo alipokutana na jopo la wajumbe watatu linaloongoza timu ya pamoja ya uchunguzi ya Shirika la Kupiga Marufuku Silaha za Kemikali OPCW la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Bw. Guterres amesema wajumbe hao wamesisitiza nia yao ya kuendeleza uchunguzi wa matukio yaliyotokea Um Housh na Khan Shaykhun kwa kina, huru, bila upendeleo, na kwa njia ya kitaalam.

    Wiki iliyopita, tume hiyo ililiarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa inaendelea kufanya uchunguzi wa matukio mawili ambayo inashukiwa kuwa silaha za kemikali zilitumika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako