Waraka maalum uliotolewa na Mahakama Kuu ya China umesema, watu zaidi ya elfu 27 wamehukumiwa, huku idadi ya kesi za uhalifu wa aina hiyo zilizofunguliwa zimefikia 16,373. Waraka huo pia umesema mahakama katika ngazi zote zimeimarisha kusikiliza kesi za raia zinazohusiana na masuala ya mazingira.
Pia, kituo cha utafiti wa sheria kuhusu rasilimali za mazingira katika Mahakama hiyo, leo kimetoa mwendelezo wa ripoti kuhusu sheria ya mazingira nchini China, na kutoa wito wa sheria kuhusu uwajibikaji na kuboresha mfumo huo kwa ajili ya usimamizi wa kufungua kesi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |