• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuwa mwenyeji wa jukwaa la kuchochea ushiriki wa vijana kwenye kilimo

    (GMT+08:00) 2017-07-14 08:42:57

    Kenya itaandaa jukwaa la kitaifa la siku tatu kujadili ushiriki wa vijana kwenye mfumo muhimu wa kilimo ikiwemo uzalishaji, uhifadhi, na soko.

    Mkurugenzi wa ngazi ya juu kutoka wizara ya kilimo nchini Kenya Bi. Anne Onyango amesema, mkutano huo utakaofanyika kuanzia jumatano ijayo, utaangalia njia mpya za kuwashawishi vijana kuchagua kilimo kama ajira yao ya kudumu. Amesema vijana zaidi ya 500 wamealikwa kushiriki katika mkutano huo unaolenga kuimarisha ushiriki wao katika kilimo cha kibiashara, na kwamba vijana hao watapata fursa ya kuonyesha teknolojia na uvumbuzi unaoleta mageuzi kwenye sekta ya kilimo.

    Bi. Onyango pia amesema Benki ya Maendeleo ya Afrika imekubali kuikopesha serikali ya Kenya dola milioni 32 ili kuwashawishi vijana kushiriki zaidi kwenye kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako