• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuboresha mazingira ya kazi ya wachimbaji wadogo

    (GMT+08:00) 2017-07-14 08:46:56

    Serikali ya Tanzania imezindua mpango wa kuboresha mazingira ya kazi ya wachimbaji wadogo kupitia mkopo wa dola za kimarekani million 3.7 uliotolewa na Benki ya Dunia.

    Akifafanua kuhusu mpango huo, Kaimu mkurugenzi wa Utafiti na Uchimbaji wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO, Alex Rutagwelela amesema mpango huo utashughulikia changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo, ikiwemo mbinu mbaya za uchimbaji madini. Ameeleza kuwa mpango huo awali utatekelezwa katika maeneo saba ya migodi nchini humo, yakiwemo Buhemba, Itumbi, Katente-Ushirombo, Mpanda, Kange, Kyerwa na Masakasa.

    Mpango huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja ambapo pia utajumuisha ujenzi wa vituo saba vya migodi vitakavyotumika kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako