• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahamiaji 6,800 waliookolewa watarajiwa kufika Italia ndani ya siku tatu

    (GMT+08:00) 2017-07-14 08:52:06

    Wahamiaji na wakimbizi 6,800 wanatarajiwa kufika nchini Italia ndani ya siku tatu, baada ya kuokolewa kwenye bahari ya Mediterranean. Kwa mujibu wa kikosi cha ulinzi wa pwani nchini Italia, watu 4,100 kati yao waliokolewa katika operesheni 20 zilizofanywa Jumatano na jeshi la majini na walinzi wa pwani ya Italia, kwa kushirikiana na jeshi la majini la Umoja wa Ulaya. Polisi nchini Italia pia wanawashikilia watu watano, wakiwemo raia wawili wa Gambia, wamisri wawili na raia mmoja kutoka visiwa vya Comoro, wanaotuhumiwa kujihusisha na magendo ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako