• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Ufaransa na Marekani wakiri kuwepo kwa maoni tofauti kwenye masuala ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2017-07-14 09:03:46

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa jana mjini Paris alikutana na mwenzake wa Marekani Donald Trump.

    Marais hao wamekiri kuwepo kwa maoni tofauti kwenye masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, lakini wanatarjia kuwa tofauti hizo hazitaathiri uhusiano kati ya nchi mbili.

    Rais Macron amesema, anaheshimu uamuzi wa rais Trump, lakini atashikilia msimamo wa kufuata makubaliano hayo, na anatarajia kuendelea kufanya mazungumzo na Marekani kuhusu suala hilo.

    Kwa upande wake, rais Trump amesema, mabadiliko huenda yatatokea katika suala la makubaliano ya Paris, na hata kama hali haitabadilika, uhusiano kati ya nchi hizo hautaathiriwa.

    Pande hizo mbili pia zimejadili masuala ya Syria na Iraq. Rais Macron amesema mbali na kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugaidi, nchi hizo mbili pia zinatarajia kutafuta utatuzi wa kisiasa wa mgogoro nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako