• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wapongeza kukombolewa kwa mji wa Mosul

    (GMT+08:00) 2017-07-14 09:31:37

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilipongeza kukombolewa kwa Mosul, mji wa kaskazini mwa Iraq, na kusema ni hatua muhimu katika juhudi za dunia za kutokomeza kundi la IS.

    Katika taarifa ya pamoja, Baraza hilo limepongeza juhudi zilizofanywa na vikosi vya usalama vya Iraq pamoja na wananchi wake katika mapambano ya kuliondoa kundi la IS nchini humo. Pia Baraza hilo limetoa mwito kwa pande husika zitekeleze wajibu wa kuwalinda wananchi katika baadhi ya sehemu za Iraq ambazo bado zimedhibitiwa na kundi la IS.

    Wakati huohuo, Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF jana limesema lina wasiwasi na afya ya watoto laki 6.5 walioishi kwenye mapigano na wengine wanaoendelea kuteseka.

    Naibu mwakilishi wa UNICEF nchini Iraq Bi Hamida Ramadhani amesema, katika siku tatu zilizopita, Shirika hilo na wenzi wake wameshuhudia kuongezeka kwa idadi ya watoto walio hatarini wanaokwenda kwenye vituo vya afya bila ya kuwa na wazazi au walezi. UNICEF imetoa wito kwa pande zote kuwapatia matibabu watoto wote na kuwapatia maisha bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako