• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gor Yajizatiti lakini walazwa na Everton

    (GMT+08:00) 2017-07-14 10:25:18
    Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia jana usiku walilambishwa sakafu na timu ya Everton kutoka Uingereza katika mechi ya kirafiki iliyochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

    Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Wayne Rooney na kiungo Kieran Dowell walipachika bao moja kila moja na kusaidia Everton kuzima Gor Mahia 2-1.

    Timu zote zilianza vizuri kabla ya Gor kuimarika. Hata hivyo, Everton ilizidi nguvu Gor, ambayo ilijikatia tiketi ya kumenyana na klabu hiyo ya Uingereza baada ya kuaibisha mahasimu wa jadi AFC Leopards 3-0 katika fainali ya shindano la SportPesa Super Cup nchini Tanzania hapo Juni 11.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako