• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda Cranes kuchuana na timu ya soka ya South Sudan

  (GMT+08:00) 2017-07-14 10:26:15
  Timu ya soka ya Uganda, maarufu kama Cranes leo usiku itamenyana na kikosi cha soka kutoka Sudan Kusini kwenye mechi ya kufuzu CHAN.

  Hata hivyo kocha mkongwe Leo Adraa, ameonya Uganda dhidi ya kudhalilisha majirani wao Sudan Kusini kwani kulingana naye timu hiyo kutoka Juba imenoa makali yake vilivyo.

  Aidha, mkufunzi huyo anadai kuwa Sudan Kusini itapata motisha ya kucheza mbele ya mashabiki wa nyumbani huku kukiwa na wingi wa imani kuwa wachezaji wengi wa nchi hiyo changa barani Afrika wanaosakata soka ya kulipwa Uganda, watakuwa wa manufaa sana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako