• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viwanda vya China na Marekani vyasaini makubaliano ya kilimo yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 5

    (GMT+08:00) 2017-07-14 17:48:06

    Viwanda zaidi ya 20 kutoka China na Marekani vimesaini makubaliano huko Iowa, Marekani, ambapo viwanda vya China vitaagiza tani milioni 1.3 za maharage na tani 371 ya nyama za nguruwe na ng'ombe kutoka Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 5.

    Konsela wa mambo ya sayansi na teknolojia wa China mjini Chicago, Marekani Bw. Xu Hai alikitoa hotuba katika sherehe ya utiaji saini wa makubaliano hayo, amesema viongozi wa China na Marekani wamefikia mpango wa siku 100 kuhusu ushirikiano wa uchumi kati ya pande hizo mbili katika mazungumzo kati yao yaliyofanyika mwezi Aprili mwaka huu, na utiaji saini wa makubaliano ya kilimo ni moja ya hatua za utekelezaji wa mpango huo.

    Naibu gavana wa jimbo la Iowa Bw. Adam Gregg amesema, kupokea nyama ya ng'ombe kwa soko la China ni jambo la kufurahisha kwa jimbo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako