• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa walitaka baraza la usalama kutoa uungaji mkono zaidi kwenye mapambano dhidi ya ugaidi Afrika Magharibi na eneo la Sahel

    (GMT+08:00) 2017-07-14 19:04:06

    Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Afrika Magharibi na Sahel Bw Mohamed Ibn Chambas ametoa mwito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutoa uungaji mkono zaidi kwenye mapambano dhidi ya ugaidi kwenye nchi za Afrika Magharibi, na kuimarisha mkakati wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Sahel.

    Bw Chambas amesema ugaidi na matumizi ya mabavu vimefanya hali ya kibinadamu kuwa mbaya, na kuharibu uhuru wa nchi za maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na Mali, Mauritania, Cameroon, Burkina Faso, Senegal, Nigeria, Niger na Chad.

    Eneo la Liptako-Gourma linalounganisha Mali, Burkina Faso na Niger, katika miezi ya hivi karibuni limeshuhudia kuongezeka kwa shughuli za kigaidiza siasa kali, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya kupanga ya kuvuka mpaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako