• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashuhudia ongezeko la mapato huku uchumi ukiboreka

    (GMT+08:00) 2017-07-14 19:04:53

    Wizara ya Fedha ya China imetoa takwimu zinazoonyesha kuwa, mwezi Juni China iliweka rekodi nzuri ya ongezeko la uchumi, kwa kuwa na ongezeko la asilimia 8.9 la mapato na kuwa dola za kimarekani bilioni 251.8, likiongezeka kutoka asilimia 3.7 ya mwezi Mei.

    Wizara hiyo pia imesema katika miezi sita ya mwanzo mwaka huu, ongezeko la mapato limefikia wastani wa asilimia 9.8, na kuwa na kasi kubwa ya wastani, ikiashiria utulivu na mwelekeo mzuri wa uchumi.

    Pato la taifa GDP liliongezeka kwa asilimia 6.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ikilinganishwa na asilimia 6.8 ya robo iliyotangulia, na kuwa juu ya makadirio ya ongezeko lililowekwa na serikali la asilimia 6.5.

    Wizara ya fedha pia imesema katika mwezi Juni matumizi yaliongezeka kwa asilimia 19.1 na kufikia yuan trilioni 2.7, yakiwa yameongezeka kutoka asilimia 9.2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako