• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Kenya watakiwa kulipa mikopo yao kabla ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-07-14 19:14:19

    Wabunge wa bunge la Kenya wametakiwa kukamilisha malipo ya mikopo yao ya nyumba kufikia Agosti 7 mwaka huu.Wabunge hao pia wanatarajiwa wawe wameondoka katikia ofisi zao za bunge na maeneo ya bunge kwa kuwa muda wa bunge hilo utakamilika Agosti 8. Hata hivyo wataendelea kutumia bima ya matibabu hadi mwisho wa mwaka hata kama hawatachaguliwa.Kwa mujibu wa karani wa bunge la seneti Bwana Jeremiah Nyegenye, kama wabunge hao hawatakuwa wamemaliza kulipa mikopo yao kufikia mwisho wa kipindi hicho, basi magari yao na nyumba zitaendelea kuwa chini ya benki ambapo mikopo hiyo ilichukuliwa na zinaweza kuuzwa iwapo watashindwa kulipa. Ripoti ya mkaguzi mkuu kuhusiana na mpango wa mkopo wa gariinaonyesha kuwa wabunge 89 walichukua mikopo kufikia juni 2016. Kuhusu pensheni, Bwana Nyegenye amesema wale waliohudumu miaka miwili na zaidi sasa wataweza kupokea fedha hizo kwa mwezi ambazo ni takriban shilingi laki 1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako