• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kutoa vibali vya ajira zaidi ya elfu 10 kuziba pengo la watumishi wa umma

    (GMT+08:00) 2017-07-14 19:14:49

    Serikali ya Tanzania imetangaza kutoa vibali vya ajira 10,184 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu.

    Akizungummza mjini Dar es Salaam, waziri wa nchi, ofisi ya rais, menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Angela Kairuki amesema agizo hilo linahusisha mamlaka za serikali za mitaa, Sekretarieti za mikoa, wakala wa serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma. Kairuki ameongeza kuwa taratibu za kukamilisha mgawo wa nafasi za ajira 4,816 zilizosalia unaendelea ili kuwezesha wizara na taasisi nyingine zilizokamilisha uhakiki wa watumishi wa umma hivi karibuni kuajiri watumishi wapya kuziba nafasi wazi zilizojitokeza.Ameeleza kuwa serikali imetoa kibali kuajiri watumishi wapya 15,000 ili kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti baada ya zoezi la uhakiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako