• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vijiji vyote Tanzania kuunganishiwa umeme

  (GMT+08:00) 2017-07-14 19:15:10

  Waziri mkuu wa Tanzania Bw.Kassim Majaliwa amesema hakuna kijiji nchini humo kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya mradi wa nishati vijijini (REA).

  Amesema Serikali ya Tanzania imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo. Akizungumza na radio China Kimataifa, Bwana Majaliwa amesema serikali inajali sana wananchi wake na tayari imetenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini humo. Amesema gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 na kusisitiza kuwa mwananchi hatawajibika katika kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwa kuwa gharama hizo zimeshughulikiwa na serikali.

  Waziri mkuu ameongeza kwamba lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako