• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waonya kuhusu kuongezeka kwa njaa katika nchi za Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2017-07-14 19:28:07

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limeonya kuhusu kuongezeka kwa njaa katika nchi za Afrika Mashariki kutokana na mvua chache zilizofanya mazao yasikomae, malisho yakauke na mamia ya mifugo kufa.

    Taarifa iliyotolewa na FAO inasema kutokuwepo kwa mvua za kutosha kwa mwaka wa tatu mfululizo, kumefanya uwezo wa familia kuhimili hali hiyo, na msaada wa haraka unahitajika.

    Kwa mujibu wa FAO maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale yaliyopata mvua nusu ya hali ya kawaida, yaliyoko kati na kusini mwa Somalia, kusini mwa Ethiopia, kaskazini na mashariki mwa Kenya, kaskazini mwa Tanzania na kaskazini na kusini magharibi mwa Uganda.

    Idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula katika nchi hizo imefikia milioni 16, ikiongezeka kwa asilimia 30 tangu mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako