• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yatoa waraka wa kisheria ili kushughulikia sheria za Umoja wa Ulaya baada ya Brexit

    (GMT+08:00) 2017-07-15 15:24:59

    Uingereza jana imetoa waraka rasmi wa kisheria ili kuzifanya sheria zilizopo za Umoja wa Ulaya ziwe sheria za nchi hiyo, na kufanya maandalizi ya mpito wa kisheria baada ya kujitoa kwenye Umoja huo.

    Waraka huo pia utaondoa Sheria ya Jumuiya ya pamoja ya Ulaya iliyotungwa na bunge la Uingereza mwaka 1971, ambao umethibitisha kanuni kadhaa zikiwemo matumizi ya sheria za Umoja wa Ulaya nchini Uingereza, na kipaumbele kutolewa kwa sheria za Umoja wa Ulaya pindi ukitokea mgongano na sheria za Uingereza.

    Wachambuzi wanasema kutolewa kwa waraka huo ni maandalizi ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya na kurudisha mamlaka ya bunge ya utungaji sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako