• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Umoja wa Mataifa alaani mashambulizi katika jiji la zamani la Jerusalem

    (GMT+08:00) 2017-07-15 16:58:48

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulizi lililofanywa na watuhumiwa watatu katika mji wa zamani Jerusalem tarehe 14 alfajiri huko Israel ambapo maafisa wawili wa polisi wameuawa na mwingine kujeruhiwa.

    Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu Stephane Dujarric amesema kuwa, tukio hili lina uwezo wa kuchochea vurugu zaidi. Pande zote zinapaswa kuwajibika ili kuepusha vurugu kupamba moto.

    Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Katibu Mkuu amefurahia Rais wa Palestina Mahmoud Abbas kulaani mara moja shambulizi hilo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuweka ahadi kuwa hali katika maeneo matakatifu huko Yerusalemu yataheshimiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako