• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa kundi la IS nchini Afghanistan auawa katika shambulio lililofanywa na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-07-15 16:59:06

    Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema kiongozi wa kundi la Islamic State (IS) nchini Afghanistan Abu Sayed ameuawa na vikosi vya Marekani vilivyofanya shambulizi mapema wiki hii.

    Kwa mujibu wa msemaji wa Pentagon Dana White kuwa, ndege za vita za Marekani zilifanya shambulio Julai 11 katika makao makuu ya kundi hilo la IS katika jimbo la Kunar na kuua pia wanachama wengine wa kundi hilo.

    Sayed ni kiongozi wa tatu wa IS nchini Afghanistan kuuawa na vikosi vya Afghanistan na Marekani katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Watangulizi wake waliuawa mwishoni mwa Julai 2016 na mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako