• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaitaka Marekani kufuata makubaliano ya suala la nyuklia la Iran

    (GMT+08:00) 2017-07-15 17:31:08

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif amesema makubaliano kamili kuhusu suala la nyuklia la Iran ni mkataba wa kitaifa, ambao serikali ya Marekani inatakiwa kuufuata.

    Bw. Zarif amesema Iran ina matumaini kwamba pande husika zitafuata ahadi kuhusu makubaliano hayo, lakini serikali ya Marekani imechukua hatua na sera zisizo sahihi, na kutoheshimu wala kuunga mkono makubaliano hayo.

    Kabla ya hapo, Iran imeihimiza Marekani kuondoa vizuizi dhidi ya Iran kwa mujibu wa matakwa ya makubaliano hayo, lakini rais Donald Trump alipofanya kampeni ya kugombea urais aliwahi kuyapinga makubaliano hayo mara kwa mara, na kusema atafuta makubaliano hayo au kufanya mazungumzo tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako