• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa awasili Saudi Arabia kwaajili ya mgogoro wa kidiplomasia wa Qatar.

    (GMT+08:00) 2017-07-16 17:46:39

    Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amewasili Jeddah, mji mkubwa wa pwani huko magharibi mwa Saudi Arabia ili kusaidia kushughulikia mgogoro wa kidiplomasia wa Qatar.

    Bwana Drian ameeleza katika mkutano na waandishi wa habari uliohudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa Saudia Adel Al-Jubeir, kuwa Ufaransa inataka hatua zichukuliwe haraka iwezekanavyo ili kuwasaidia familia zinazoundwa na wake na waume kutoka nchi mbili ambao sasa wametengwa na wanafunzi wanaosoma ng'ambo.

    Le Drian amezihimiza Saudi Arabia, Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na Misri zilizositisha uhusiano wa kidiplomasia na Qatar kutatua mgogoro unaoendelea kupitia majadiliano.

    Naye Bwana Al-Jubeir amesema anaweza kutoa ushahidi kwamba Qatar ilikiuka mkataba wa Riyadh wa 2013 na mkataba wa ziada wa Riyadh wa 2014, wote ambao unalenga kuongeza ushirikiano kati ya mataifa ya Ghuba na kuepuka kuingilia kati katika mambo ya ndani ya nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako