• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq yakanusha nia ya kuingilia kijeshi nchini Syria ili kupambana na IS

    (GMT+08:00) 2017-07-17 08:58:08

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iraq Bw. Ahmad Jamal amekanusha nia ya nchi hiyo kuingilia kijeshi nchini Syria kwa lengo la kupambana na kundi la kigaidi la Islamic State. Akihojiwa na televisheni ya Al-Arabiya ya Saudi Arabia, Bw. Jamal amesema katiba ya Iraq inaizuia nchi hiyo kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine. Hivi karibuni Iraq imepata ushindi mkubwa katika kuukomboa mji wa Mosul kutoka kundi la IS, lakini maeneo kadhaa nchini humo bado yanadhibitiwa na kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako