Waziri wa fedha wa Uingereza Bw Philip Hammond, amesema Uingereza inapaswa kufikia makubaliano ya mpito na Umoja wa Ulaya, ili kuyapatia makampuni muda wa mpito ili isije ikatokea hali ya kuondoka ghafla kutoka Umoja wa Ulaya.
Bw. Hammond alipohojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC amesema wiki kadhaa zilizopita kulikuwa na wazo jipya la kuweka muda wa mpito kwa Brexit, lakini kwa sasa watu wengi wanakubalia wazo hilo. Kuweka muda wa mpito kutaifanya Uingereza itumie mpango wa sasa ipasavyo, ili kupunguza athari kwa uendeshaji wa makampuni.
Waziri wa Brexit wa Uingereza David Davies atakwenda Brussels leo, kufanya mazungumzo ya duru ya pili na Umoja wa Ulaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |