• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Misri na Ufaransa wajadili suala la Libya kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2017-07-17 10:10:39

    Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wamezungumza kwa njia ya simu kuhusu suala la Libya.

    Msemaji wa Ikulu ya Misri Bw. Alaa Youssef ametoa taarifa ikisema, marais hao wanaona kutatua suala la Libya na kurejesha hali ya amani na utulivu kwa njia ya kisiasa, ni muhimu kwa usalama wa kanda hiyo.

    Taarifa pia imesema, rais al-Sisi amesema juhudi za jumuiya ya kimataifa ni muhimu katika kumaliza vita na mgogoro wa Mashariki ya Kati.

    Kwa upande wake rais Macron amesisitiza kuwa Ufaransa na Misri zinatakiwa kuimarisha mazungumzo na ushirikiano katika masuala ya kimataifa na ya kikanda yanayofuatiliwa na pande mbili, hasa katika suala la Libya.

    Mbali na hayo, rais al-Sisi amesema, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaimarika, na ametaka kukuza uhusiano na kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako