• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yakosa kutamba katika mashindano ya chipukizi

  (GMT+08:00) 2017-07-17 10:34:45

  Afrika Kusini ndiyo mabingwa wapya wa Riadha za Chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18.

  Kikosi cha nchi hiyo ilimaliza mashindano hayo yaliyoandaliwa jijini Nairobi juu ya jedwali la mataifa 131 kwa medali tano za dhahabu, tatu za fedha na tatu za shaba.

  China ilimaliza katika nafasi ya pili ikifuatwa na Cuba kwenye nambari ya tatu baada ya kujizolea medali tano za dhahabu, lakini wakatofautiana katika idadi ya nishani za fedha na shaba.

  Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya mashindano haya, Mwenyeji Kenya ilimaliza nje ya nafasi tatu za kwanza. Kenya ilimaliza katika nafasi ya nne baada ya kujizolea medali nne za dhahabu, saba za fedha na shaba nne.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako