• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya KPL All Stars kutoka Kenya yaelekea Uhispania

  (GMT+08:00) 2017-07-17 10:36:37

  Timu ya KPL All Stars inayodhaminiwa na SportPesa iliondoka nchini Kenya jumapili usiku kuelekea Uhispania kushiriki mechi za kirafiki dhidi ya vilabu vya Cordoba na Sevilla Atletico wiki hii.

  Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 18 wa kucheza nyumbani waliochaguliwa na kocha wa Harambee Stars Stanley Okumbi na kocha anayefunza timu ya wachezaji wa Kenya wasiozidi miaka 20 John Kamau.

  Kikosi hicho kilichosafiri kinaonekana na wengi kama timu ambayo kitawakilisha Kenya katika michuano ya mataifa ya Afrika CHAN mwaka ujao na Okumbi anatarajia kwamba mechi hizo mbili zitawapa uzoefu unaohitajika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako