• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Njia ya kuondoa umaskini ya kaunti ya Libo, Mkoani Guizhou, China

    (GMT+08:00) 2017-07-17 17:56:32

    Kaunti ya Libo Mkoani Guizhou, China ni kaunti yenye vivutio vingi vya kimaumbile ambayo asilimia 93 ya idadi ya wenyeji wa kaunti hiyo ni watu wa makabila madogomadogo. Lakini kaunti hiyo ilikuwa tatizo kubwa kwa mkoa huo katika kuondoa maskini. Serikali ya kaunti hiyo ilipanga kuendeleza kaunti hiyo kwa kuzingatia rasilimali yao ya asili na kunufaisha wenyeji wa huko kwa kuendelea utalii…….na maelezo zaidi:

    Mwaka 2007, msitu aina ya Karst wa kaunti hiyo umekuwa eneo la urithi wa kimaumbile wa dunia. Ingawa kaunti hiyo imepata sifa hiyo nzuri, lakini, kutokana na milima mitatu inayoizunguka, miundombinu duni imekuwa tatizo la kwanza linalozuia maendeleo ya kaunti hiyo.

    Mkurugenzi wa idara ya habari wa kaunti hiyo Bw. Lei Da amesema, kuendeleza utalii ni njia pekee mwafaka itakayosaidia watu kuondokana na umaskini. Amesema, katika kaunti ya Libo kuna makabila ya Buyi, Shui, Miao na Yao, hivyo, ni bora waendeleze utalii kwa kuzingatia utamaduni wa makabila ili kuvutia watu wengi zaidi. Walitoa utalii wa kutembelea kijiji, kuishi na wanakijiji na kutembelea kabila la wa-shui.

    Bibi Luo Ting ni mwanamke kutoka kabila la Shui ambaye anafanya kazi katika hoteli ya wanakijiji katika kijiji cha kabila la Shui. Alisema, zamani, vijana wa kijiji hicho walifanya kazi nje ya kijiji. Lakini sasa, wanapenda kurudi na kufanya kazi hapahapa ili kutunza watoto, wazazi na familia kwa urahisi.

    Naibu mkurugenzi wa kituo cha vyombo vya habari vya kisasa Cheng Xinglu amesema, mwaka 2015, kaunti ya Libo ilitoa mkakati wa maendeleo ya utalii wa eneo zima ili kusaidia watu kuondokana na umaskini na kuboresha uwiano wa maendeleo ya vijiji mbalimbali. Alisema mkakati huo unalenga kupanua nguvu bora ya kila sehemu. Kama vile, baadhi ya sehemu zinafaa kuendeleza utalii wa kutembelea makabila, nyingine zinafaa kuwa na utalii was kuishi na wanakijiji. Maendeleo ya utalii pia yanaweza kuhimiza maendeleo ya kilimo na sekta ya huduma.

    Kaunti hiyo imeunganisha utengenezaji wa mazao ya kilimo na kazi ya kuokota matunda pamoja na utalii, na kujenga bustani ya kilimo ili kuwawezesha watalii kujaribu kwenye kazi ya kilimo. Hivi sasa, kaunti hiyo ina bustani 5 zenye ufanisi za kilimo na moja ya teknolojia. Bidhaa zilizotolewa na bustani hizo ni pombe, matunda na nguo na zimeleta mapato ya yuan bilioni 4.69.

    Chini ya mkakati huo mzuri, mwaka 2016, kaunti hiyo ilipokea watalii milioni 11.08. Idadi hiyo imeongeza kwa asilimia 43.23, ililinganishwa na mwaka jana. Pato la utalii lilifikia yuan bilioni 11.1. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, idadi ya watalii imeongeza kwa asilimia zaidi ya 60. Bw. Lei Da amesema, mwaka huu, kaunti hiyo imewekeza yuan bilioni 8.8 kuboresha utalii wa kanda hiyo na kujitahidi kutimiza lengo lao la kuondoa umaskini kabla ya mwaka 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako