• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu wanne wafariki baada ya jengo moja kubomoka kusini mwa Ethiopia

  (GMT+08:00) 2017-07-17 18:30:33

  Watu wanne wamefariki na wengine 11 kujeruhiwa baada ya jengo moja kubomoka mjini Arba Minch, kusini mwa mji wa mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

  Shirika la habari la Ethiopia limesema, watu waliofariki ni wapangaji wa jengo hilo la ghorofa mbili ambalo ni nyumba ya kulala wageni na idadi ya watu isiyofahamika wamenasa kwenye kifusi cha jengo hilo.

  Mkuu wa mji wa Arba Minch Ezo Emaqo amesema, mmiliki wa jengo hilo anashikiliwa na polisi kwa kosa la kujenga jengo lisilokidhi viwango, ambacho ni chanzo cha kuanguka kwake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako