• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini yatoa mapendekezo kwa Korea Kaskazini kuhusu kufanya mazungumzo juu ya mambo ya kijeshi

    (GMT+08:00) 2017-07-17 20:10:57

    Korea Kusini leo imetoa mapendekezo kwa Korea Kaskazini kuhusu kufanya mazungumzo ya mambo ya kijeshi na mazungumzo ya kazi ya shirika la msalaba mwekundu kati ya mwezi huu na mwezi ujao.Taarifa iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Korea Kusini inasema, nchi hiyo inapendekeza majadiliano kati yake na korea Kaskazini kuhusu kusitisha vitendo vyote vinavyoongeza hali ya wasiwasi karibu na mpaka wa kijeshi wa nchi hizo. Korea Kaskazini bado haijajibu kama inakubaliana na mapendekezo ya Korea Kusini.Akizungumzia hatua hiyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China inazitaka Korea Kaskazini na Korea Kusini zifanye juhudi kwa pamoja, ili kuweka mazingira mazuri yatakayorejesha upya mazungumzo kati yao ambayo yamesitishwa. Vilevile ameitaka jumuiya ya kimataifa ielewe na kuunga mkono juhudi za nchi hizo mbili na kuonesha umuhimu wa kiujenzi kwa ajili ya utatuzi wa suala la nyukilia la peninsula ya Korea.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako