• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Duru ya pili ya mazungumzo ya Brexit yafanyika Brussels

  (GMT+08:00) 2017-07-18 10:12:07

  Duru ya pili ya mazungumzo ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya imefanyika katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya huko Brussels.

  Pande mbili zinajadili ajenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na gharama za Uingereza kujitoa Umoja huo, uhakikisho wa haki na maslahi ya raia wa Umoja wa Ulaya na Uingereza wanaoishi katika upande mwingine, na suala la mpaka wa Ireland Kaskazini.

  Waziri wa Uingereza anayeshughulikia mambo ya kujitoa Umoja wa Ulaya Bw. David Davis amesema sasa ni wakati wa kujadili mambo halisi na anayataka mazungumzo hayo yafanikiwe. Mwakilishi mkuu wa kamati ya Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo Bw Michel Barnier amesema wanachunguza masuala ya msingi, ambapo wanatakiwa kuzingatia na kulinganisha misimamo ya pande mbili ili kuweza kupata maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako